19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 277584
Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias amemteua Lucas Papademos kuwa Waziri Mkuu wa serikali mpya ya mpito ya nchi hiyo.
Papademos ambaye ni mwanauchumi anachukua nafasi George Papandreou ambaye amekubali kujiuzulu baada ya kuelemewa na matatizo ya kiuchumi yanayotishia mustakabali wa nchi hiyo. Taarifa kutoka ofisi ya Rais Papoulias imesema kuwa baraza jipya la mawaziri litaapishwa kesho alasiri. Waziri Mkuu mpya atakuwa na jukumu la kuhakikisha Ugiriki inarudi katika hali nzuri ya kiuchumi na masharti yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya ili nchi hiyo ipate mkopo yanatekelezwa. Ugiriki imetakiwa kupandisha kiwango cha kodi kama sharti la kupewa mkopo zaidi na Umoja wa Ulaya EU, jambo ambalo wananchi wa nchi hiyo wanalipinga vikali.